STD 4 KISWAHILI TEST1 Please enter your email: Jaza mianya kwa majibu sahihi kwa swali 1-15. Kuku ——1—– mayai —–2 ——sana. Mayai hayo yaliwekwa kwenye choto kisha —-3—-kwa muda wa —–4—— matatu hivi kisha —5—- vifaranga —6—- walikuwa na rangi tofauti. Kuku alilinda vifaranga —-7—– wasiliwe na —-8—– Siku —-9—– kuku aliwaficha vifaranga kwenye mbawa —–10—— . Mwewe naye alifanya ujanja na kuangusha punje —–11—- mahindi karibu. Kuku —–12—– na kuangukia kwenye mlo wake. Kuku huyo ——-13—– mahindi kwa furaha bila kufahamu ujanja wa mwewe. Mwewe aliwavaMia vifaranga na kumchukua —–14——-. Kuku alimlilia kifaranga wake lakini kilio si —–15—. MAJIBU 1. A. alizaa B. aliangua C. alitaga D. aliteka 2. A. mengi B. mingi C. wengi D. mwingi 3. A. aliyalalia B. akayaatumia C. akayavamia D. akayakalia 4. A. wild B.juma C.miezi D. majuma 5. A. yakaanguliwa B.yakaliwa C.ambaye D. ambao 6. A. ambavyo B.ambayo C.ambaye D. ambao 7. A. wake B.vyake C.vyao D. zao 8. A. jogoo B.mbuni C.mwewe D. njiwa 9. A. mmoja B.kimoja C.moja D. monja 10. A. yake B.zake C.yao D. lao 11. A. la B.ya C. za D. wao 12. A. alipuruka B.alianguka C.alidandia D. alizama 13. A. alitafuna B.alikekela C.aliyadona D. aliyagegeda 14. A. kimoja B.rnmoja C.moja D. wamoja 15. A. kizuri B.dawa C.tatizo D. kibaya Jibu maswali nambari 16 – 30 kwa ukifuata maagizo yaliyotolewa. 16. Andika sentensi hii katika wingi; Ubao utavunjika A. Bao zitavunjika B. Mabao yatavunjika C. Bao yatavunjika D. Mbao zitavunjika 17. Kanusha; Sisi hula asubuhi. A. Sisi hatukuli asubuhi B. Sisi hatulangi asubuhi C. Sisi hatuli asubuhi D. Sisi hukula asubuhi 18. Alinunua kalamu wino ———– mwekundu. A. chenye B. mwenye C. lenye D. yenye 19. Chagua kiulizi sahihi; Amefungua mlango kwa ufunguo A. upi B. lipi C. ipi D. zipi 20. Daktari huitwa tabibu au A. muuguzi B. nesi C. mganga D. mchawi 21. Chagua kiambishi sahihi. Chungu –ko mekoni. A. i B. li C. u D. ki 22. Jaza pengo; Wayo ni kwa mwanadamu, ————- ni kwa ng’ombe. A. kiatu B. mguu C. teke D. kwato 23. Kamilisha methali ifuatayo. Baada ya kisa ni ——-. A. faraja B. kifo C. mkasa D. kitendo 24. Jina `dawati’ liko katika ngeli gani? A. LI-YA C. U-ZI B. I-ZI D. YA – YA 26. . Tegua kitendawili kifuatacho Nyumba ya baba Ma wageni wengi. A. Soko C. Shule B. Kanisa D. Ulimwengu 27. Tunaliitaje jiko la makaa? A. Meko B. Stima C. Seredani D. Dohani 28. Mtu asiyeweza kusikia huitwaje? A. Kipofu B. Kiwete C. Kibyongo D. Kiziwi 29. Kinda ni mtoto wa ———- A. ndege B. kuku C. nyoka D. mbwa Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 31 – 40. Hapo zarnani wanyama walikuwa wakishiriki katika michezo mbalimbali mara moja kwa mwaka. Wakati huu wa michezo, kila mnyama, ndege na hata samaki walikuwa wanaalikwa na mfalme tembo. Wanyama hawa walikuwa wanashiriki katika michezo mbalimbali kama vile kushindana mbio, kuogelea, kupigana ngumi na mateke na michezo mingineyo. Pundamilia alikuwa anashinda kila mara katika mchezo wa kupigana mateke. Mbuni naye alikuwa akishindana mbio zote. Rekodi ya papa katika kuogelea iliwashinda wengi kuivunja. Kila mwaka, rnheshimiwa kinyonga alikuwa akialikwa kuja kushabikia mchezo wake wa kupigana ngumi na mateke. Alikuwa akiupenda kama chanda na pete. Katika mchezo huu, kinyonga alipata maarifa rnengi hasa siku ile. Pundamilia alimshinda simba kwa kumpiga teke lililomuumiza. Michezo ilipofika kikomo saa kumi na moja siku hiyo, washindi wakatangazwa na katibu bwana Ngiri na kutuzwa zawadi kochokocho. MASWALI 31. Wanyama walikuwa wakifanya michezo mara ngapi kwa mwaka? A. Mbili B. Moja C. Tano D. Kumi 32. Kulingana na taarifa ni mchezo upi ambao haukupendwa na wanyam? A. Kuogelea B. Mbio C. Kupigana D. Kuimba 33. Ni nani aliyekuwa mshindi katika mchezo wa kupigana mateke? A. Pundamilia B. Nyumbani C. D. Mwituni 34. Kulingana na hadithi, makao yake papa ni wapi? A. Mitini B. Nyumbani C. Majini D. Mwituni 35. Ni wakati gani katika michezo ambao kinyonga alipata maarifa mengi? A. Pundamilia alipomshinda simba B. Simba alipomshinda pundamilia C. Papa alipoogelea akashinda D. Mbuni alipomshinda ngiri. 36.Mbuni alipokea zawadi kwa kushinda mchezo upi? A. Kuogelea B. Mbio C. Kuimba D. Kucheza 37. Neno `kochokocho’ limetumika katika ufahamu. Neno hii lina maana ya A. chache B. ndogo C. kwa wingi D. tele 38. Ni nani aliyekuwa katibu wa mchezo mwaka huo? A. Papa B. Kinyonga C. Ngiri D. Ndovu 39. Neno lenye maana sawa na ‘tembo’ ni A. ndovu B. simba C. mbuni D. papa 40. Kichwa mwafaka cha hadithi hii ni A. Hapo zamani B. Wanyama na rnbuni C. Siku ya michezo ya wanyama D. Kupigana mateke Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 41 – 50. Nyoteyo ni msichana mwenye umri wa miaka kumi na miwili. Ana bidii sana masomoni, hates wanafunzi wanzake humwita `nyota’. Nyoteyo hana wazazi, yeye ni yatima. Yeye ni mwanafunzi katika shule ya msngi ya Naelewa. Wazazi wake waliaga dunia walipovamiwa na wezi nyumbani kwao miaka mitatu iliyopita. Yeye huishi na mjomba wake.Nyoteyo hupenda rafiki safe. Hapendi kukaa na watoto wachoyo, wachafu, wanaonuka kama beberu, wezi na wasiofanya kazi za walimu. Hupenda kusoma vitabu vingi vya kiswahili na hadithi nzuri. Yeye husema kuwa akimaliza masomo yake angependa kuwa mhubiri iii awahubirie watu amani. Jambo hili ni tofauti na mahitaji ya wenzake. Kwa kweli hapendi vita. Yeye ni mpole kama mwanakondoo. Huwauliza walimu wake maswali katika masomo yake. Sasa Nyoteyo ndiye kiranja wa darasa lake la tano. Alichaguliwa na mwalimu wake Bwana Furaha kwa sababu ya tabia zake za kuwapendeza wengi. Ni wangapi wangetamani kuwa na tabia kama za Nyoteyo? MASWALI: 41. Nyoteyo alikuwa na miaka mingapi wazazi wake walipokufa? A. Kumi na miwili B. Sita C. tisa D. Kumi 42. Ni akina nani waliowaua wazazi wa Nyoteyo? A. Majabazi B. Wezi C. Wachawi D. Askari 43. Nyoteyo hapendi A. wanafunzi wanaofanya kazi ya mwalimu B. wanafunzi wanaonukia C. wanafunzi wasiooga D. wanafunzi wanaowatii walimu wao 44. Kulingana na hadithi hii ni kweli kuwa A. Nyoteyo ni msomaji bora wa vitabu vya kiswahili B. Nyoteyo si yatima C. Nyoteyo anaishi peke yake kwake D. Nyoteyo hupenda kukaa na wanafunzi wachoyo 45. Nyoteyo ni mpole kama A. maji C. yatima B. mwanakondoo D. wazazi wake 46. Tunamaanisha nini tunaposema kuwa ” Nyoteyo ni yatima” A. Hapendi wanafunzi wabaya B. Yeye ni mwerevu na hana hatia C. Anasoma kwa bidii D. Hana wazazi 47. Nyoteyo anatamani kuwa nani atakamaliza masomo yake? A. Daktari B. Mwimbaji C. Msomaji D. Mhubiri 48. Nani aliyemchagua Nyoteyo kuwa kiongozi wa darasa lake ? A. Wanafunzi B. Bwana Furaha C. Kiranja D. Wazazi 49. Nyoteyo alikuwa akiishi kwa —————— wake A. rafiki B. mjomba C. mwalimu D. wanafunzi 50. Hadithi hii inatufundisha nini? A. Usiposoma utapita. B. Tuwe na upendo na amani maishani C. Kila mwanafunzi ni yatima. D. Tusiwaulize walimu maswali mengi Loading … Question 1 of 48