STD 8 KISWAHILI TEST2 Please enter your email: Kiswahili ni mojawapo ya lugha………….1…………wazungumzaji wengi. Lugha ya Kiswahili …………..2……. zama za ukoloni…………3……..Waafrika dhidi ya wakoloni. Hatua ya kukifanya Kiswahili lugha rasmi nchini Kenya ……..4………..hadhi ya lugha husika. ………..5……………hapo awali, tunatarajia Kiswahili kutumiwa ………6………… na Kiingereza katika shughuli za kiofisi. Hata hivyo, ……………7………… patakuwa na haja ya kutafsiriwa kwa makala mengi kwa Kiswahili. 1.MAJIBU A. Vyenye B. Zenye c. Wenye D. Chenye 2. MAJIBU A. ingekuwa imetumiwa B. ilikuwa imetumiwa C. ingekuwa ikitumiwa D. ilikuwa ikitumiwa 3. MAJIBU A. kuwatambulisha na kuwaunganisha B. kuwahamasisha na kuwalinganisha C. kuadumisha na kuwajenga D. kuwastaiisha na kuwalenga 4. MAJIBU A. imeieneza B. imeitia fora C. imeikweza D. imeivika kilemba 5. MAJIBU A. Licha ya B.. Bighairi ya C. Mbali na D. Kinyume na 6. MAJIBU A. mtawalia B. mkabala C. sadakta D. sambamba 7. MAJIBU A. hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe B. hakuna rnarefu yasiyokuwa na ncha C. hakuna bamvua lisilo usubi D. hakuna kubwa lisoshindwa Mtoto ana haki ………8…….. Anastahili …..9……… vizuri iii kuifaa jamii ……..10….. Tabia ya mtoto ……….11……. na jamii, hivyo tunaweza kudai kuwa mtoto ni zao la jamii. ……12……. mtoto ana haki ya lishe bora ……13……nguvu, yaani,……14….., na kumwezesha kujikinga na maradhi kama vile ……..15…... Ugonjwa huu husababishwa na kula chakula ambacho kina upungufu wa viinilishe. 8.MAJIBU A. maradufu B. akali C. anuwai D. maridhia 9. MAJIBU A. kukidhiwa B. kutunukiwa C. kuengaengwa D. kutunzwa 10. MAJIBU A. yetu B. yake C. yangu D. yenu 11. MAJIBU A. huathirika B. huathiria C. huathiriana D. huathiriwa 12. MAJIBU A. Aidha B. Aghalabu C. Yamkini D. Pengine 13. MAJIBU A. litakaompa B. itakapompa C. litakalompa D. itakayompa 14. MAJIBU A. azma B. ilhamu C. siha D. hima 15. MAJIBU A. safura B. utapiamlo C. surua D. tetekuwanga Kutoka swali la 16 rnpaka 30, chagua jibu lililo sahihi. 16. Maneno yafuatayo yanafuatana vipi katika kamusi? (i) muhibu (ii) muhtasari (iii) muhali (iv) muhula A. (iii), (ii), (i), (iv) B. (iii), (i), (ii), (iv) C. (iv), (i), (ii), (iii) D. (iv), (ii), (i), (iii). 17. Umoja wa: “Nywele zao ndefu ziliwavutia.” ni: A. Nywele yake ndefu iliwavutia B. Nywele zake ndefu zilimvutia C. Unywele wake mrefu uliwavutia D. Unywele wake mrefu ulimvutia. 18. Chagua jibu lenye nomino zilizo katika ngeli ya i-i pekee. A. kahawa, fedha B. chumvi, chupa C. mali, chai D. sukari, mvua 19. Ni jibu lipi lenye maelezo sahihi? A. Muundi ni sehemu ya mkono kuanzia begani hadi kwenye kiwiko. B. Kitengele ni sehemu ya mwisho ya mkono yenye vidole. C. Nyonga ni sehemu ya juu ya kiuno. D. Paji ni sehemu ya juu ya kichwa. 20. Hisani ni kwa wema na kunadi ni kwa: A. kuuza B. kutangaza; C. kusambaza; D. kuchuuza 21. Chagua kinyume cha: Wageni waliwasili kabla ya eropleni kupaa. A. Wenyeji waliondoka baada ya eropleni kutua B. Wenyeji waliondoka kabla ya eropleni kutua. C. Wageni waliondoka kabla ya eropleni kutua. D. Wageni waliondoka baada ya eropleni kutua. 22. Tikiti, limau na fenesi ni matunda ilhali wimbi, mahindi na mtama ni: A. miti; B. vyakula; C. nafaka; D. mbegu. 23. 6/9 kwa maneno A. sudusi sita; B. tusui sita; C. tusui tisa; D. sudusi tisa. 24. Kukanusha kwa: “Nyungu iliyonunuliwa iliuzwa tena,” ni: A. Nyungu iliyonunuliwa haijauzwa tena B. Nyungu iliyonunuliwa haikuuzwa term C. Nyungu isiyonunuliwa haijauzwa tena D. Nyungu isiyonunuliwa haikuuzwa tena. 25. Ni jibu lipi ambalo si aina ya shairi? A. kibwagizo; B. tathlitha; C. ngonjera; D. tarbia. 26. Onyesha sentensi yenye kielezi cha A. Hukimbizana mara kwa mara. B. Wanafunzi watafuzu mwakani. C. Katabo alisafiri kwa gari. D. Tulielekezwa pembezoni 27. Kiambishi `ka’ katika sentensi: “Alienda shuleni akasome Kiswahili;” kinaonyesha: A. kufuatana kwa matukio; B. kulazimika C. kusudi D. kutegemeana kwa matendo. 28. Chagua kundi Iinaloonyesha kitenzi .kilichoundwa kutokana na kivumishi. A. Mvumilivu uvumilivu; B. Mwaminifu aminika; C. Mapishi pikika; D. Wacheshi ucheshi. 29. Kitara ni upanga mwembamha wa kuongozea gwaride. Kitara vile vile ni: A. sehemu iliyotengenezwa kukaushia mbegu; B. chombo kitumiwacho kufungia mlango; C. nazi changa ambayo haijawa dafu; D. sehemu inayopandwa mimea au miche. 30. Chagua sentensi ambayo imetumia `na” kama kiunganishi. A. Wafanyakazi wote wameitwa na nokoa shambani. B. Wafanyakazi waliokuja wanajulikana na nokoa wao. C. Wafanyakazi na nokoa wao wanalima shamba D. Wafanyakazi walikuwa na matumaini ya kumwona nokoa. Soma kifingu kifilatacho kisha ujihu maswali 31 mpaka 40 Kuna aina mbili kuu za misitu. Ipo ile ya kiasili kama vile Msitu wa Karura na Msitu wa Mau. Hali kadhalika, ipo misitu ya kupandwa kama ile ya Kinale na Webuye. Misitu ni hazina kubwa kwa jamii yoyote ile. Kila mwanajamii anapaswa kujivunia misitu. Misitu husheheni miti ya aina nyingi ambayo, pamoja na kuwa makazi ya wanyama, hutoa vyakula kama vile matunda na majani ambayo huwafaidi binadamu na viumbe wengine. Bila misitu binadamu na wanyama wangeangamia. Misitu ni kivutio cha watalii. Watalii kutoka ndani na nje ya nchi huzuru misitu na mbuga mbalimbali za wanyama kuajabia uzuri wake. Watalii hawa hulipa fedha za kigeni ambazo hutumiwa kuanzishia miradi ya kiuchumi kama vile kustawisha miundomsingi. Fauka ya hayo, misitu husafisha hewa na kurembesha mandhari wanamoishi binadamu. Rangi ya kijani kibichi na maua yenye rangi tofautitofauti huyafanya mazingira kupendeza hata yakitazamwa kwa mbali. Mandhari yasiyo na miti hayakosi urembo tu, bali huwa wazi kiasi kwamba hata mapaa ya majengo yaliyo hapo wakati mwineine hupeperushwa na upepo mkali. Vipindi virefu vya jua huwanyima viumbe starehe na huweza kusababisha saratani ya ngozi kwa binadamu. Miti hufanya vivuli ambavyo huwakinga watu na wanyama dhidi ya miale ya jua. Isitoshe, si ajabu kuwa mahali ambapo pana miti mingi kwa kawaida hupata mvua hata wakati usio wa majira ya mvua kwingineko. Sekta ya tiba imefaidika si haba kutokana na miti. Matabibu wa kienyeji na hata wa kisasa hutumia mizizi, majani na magome ya miti kutengenezea dawa. Miti kama vile mwarubaini hutibu magonjwa mengi. Hivi rasa magonjwa kama vile bolisukari, shinikizo la damu na ugonjwa wa figo yarneweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa zinazotokana na miti. Inasemekana kuwa hata nyoka humtibu nyoka mwenzake kwa majani! Miti hutumiwa viwandani kutengenezea bidhaa kama vile karatasi na samani. Viwanda hivi hutoa ajira kwa maelfu ya raia, hivyo kupunguza makali ya uhaba wa nafasi za kazi nchini. Ni wazi kuwa uhifadhi wa misitu una manufaa tumbi nzima kwa binadamu. Hata hivyo, binadamu mwenyewe ndiye anayeiangamiza misitu yenyewe. Watu wenye mate ya fisi wamekata miti kiholela kwa ajili ya kupata kuni na kuchomea makaa ya kuuza. La kusikitisha ni kwamba watu hawa hawadiriki kupanda miti mingine kufidia ile waliyoikata. Wengine, kwa kutojua wanajipalia makaa, hupanda miti ambayo inakausha vyanzo vya maji na kuchangia kuenea kwa kasi kwa jangwa. Hali kadhalika, wapo warina asali ambao katika juhudi zao za kurina husababisha kuteketea kwa misitu. Kifungu cha katiba kinachohusu mazingira na mali ya asili kinasisitiza suala la uhifadhi wa mazingira. Kila mwanajamii basi ana jukumu la kuilinda misitu na kuepuka mazoea ambayo yanaiangamiza, la sivyo tutakuwa tunajichimbia kaburi. MASWALI 31. Kulingana na kifungu, mchango wa utalii kwa jumla ni: A. kuongeza fedha za kigeni kwenye mbuga B. kuboresha miundomsingi kwenye misitu C. kuimarisha uchumi wa nchi; D. kuwekeza miradi ya nchi. 32. Chagua hasara za kutohifadhi misitu kwa mujibu wa kifungu. A. kunyauka kwa majani, kupoteza urembo B. kuporomoka kwa majengo, kupoteza mvuto; C. mahali pakavu, kuchukiza kwa mazingira D. upepo mkali, kunyauka kwa maua. 33. Ni jibu lipi sahihi kulingana na kifungu? A. Dawa za kienyeji huponya kabisa magonjwa mengi sugu. B. Kuhifadhi misitu kunaweza kuchangia kuongezeka kwa nafasi za kazi. C. Mahali penye miti mingi hupata mvua inayotegemewa kila mara. D. Kuwa na vipindi vya jua kali kunaweza kusababisha saratani. 34. Kifungu kinasema kuwa miti hutumiwa: A. kutengenezea kawi na kuwasetiri viumbe B. kuunda samani na kuhifadhi maji; C. kusafishia hewa na kufanikisha majengo D. kuvuta mvua na kuburudisha viumbe. 35. Manna ya methali, “Mwiba wa kujichoma hauambiwi pole,” imedhihirika katika kifungu kwa vile: A. Watu ndio wanaojisababishia hali mbaya ya ukame kwa kupuuza umuhimu wa miti. B. Watu ndio wanaojisababishia hali mbaya ya kiangazi kwa kupuuza umuhimu wa misitu. C. Watu ndio wanaojikaushia visima kwa kupanda miti isiyofaa. D. Watu ndio wanaojichomea misitu kwa kurina pasipostahili. 36. Mwandishi anaonyesha kuwa kichocbeo kikuu cha kukata miti ni: A. kuwa na haja ya kuuza makaa; B. kuwa na hamu ya kupata asali; C. kuwa na tamaa ya mali; D. kuwa na mahitaji ya kuni. 37. Ni jibu lipi ambalo si sahihi kulingana na aya ya nane? A. Ukataji miti unapaswa kuandamana na upandaji miti upya B. Shughuli yenye faida huweza kuishia kuwa janga. C. Ukosefu wa maarifa unaweza kusababisha hasara. C. Ukosefu wa maarifa unaweza kusababisha hasara. 38. Kulingana na aya ya mwisho: A. Mazingira huhifadhiwa kupitia kwa kifungu cha katiba. B. Mwanajamii hujiletea majuto kwa kutoepuka mienendo isiyokubalika C. Mazingira huharibiwa na hulka zisizofaa za binadamu. D. Mwanajamii anastahili kufuata mshawasha wa katiba. 39. Kwa mujibu wa taarifa, `yameweza kudhibitiwa’, ina manna: A. Yameweza kuondolewa; B. Yameweza kuzuiliwa; C. Yameweza kutibiwa yote; D. Yameweza kupunguzwa yote. 40. Manna ya, `hawadirikr, kulingana na kifungu ni: A. bawawahi; B. hawaambulii; C. hawarauki; D. hawawazii. Soma kifingu kifuatacho kisha ujthu maswali 41 mpaka 50. Tenga alilelewa katika mazingira yaliyojaa neema, furaha na uchangamfu. Wazazi wake Bwana Mtanga na Bi. Zuhura walikuwa wakwasi wa kutajika katika janibu hizo, si kwa mali tu bali kwa nyoyo zao zilizokuwa tayari kila mara kuwakirimu wanalujiji kwa lolote. Bwana Mtanga na Bi. Zuhura hawakulala maskini wakaamka matajiri. Mtanga alianza kazi kama tarishi katika Makavazi ya Umma. Ingawa hii ilikuwa kazi ya kijungu jiko mekoni, Mtanga hakwenda nguu; alijitahidi kwa vyovyote vile kujinyanyua. Akajisajili kwa kozi mbalimbali za usimamizi wa makavazi na kuhitimu vyeti tofautitofauti vikiwemo stashahada na shahada katika masuala ya usimamizi wa mashirika ya umma. Jitihada zake zikazaa matunda. Akapandishwa cheo mwaka baada ya mwingine hadi akawa msimamizi wa Makavazi ya Umma. Baadaye akaajiriwa na shirika la Msalaba Mwekundu kama Mkrurugenzi wa Huduma za Kijamii. Bi. Zuhura naye, baada ya kuhitimu masomo ya shule ya upili, alisomea taaluma ya ukutubi na baadaye kuajiriwa katika maktaba ya chuo kikuu cha Tungama. Hapa Zuhura alitambua kuwa amepata nafasi adimu ya kuutia makali ubongo wake. Akajisajili kwa kozi ya ukutubi na kuhitimu shahada ya daraja la kwanza katika taaluma hii. Wakuu wake kazini wakavutiwa na juhudi zake na kumpandisha cheo, akawa Mkutubi Mkuu. Wakati Bwana Mtanga na Bi. Zuhura walipokuwa wakijiendeleza kitaaluma na kiuchumi, Tenga naye alikuwa anajikulia tu kama uyoga bila mpalilizi. Nyadhifa za wazazi wake zilimpokonya Tenga ushirika wa wazazi wake. Ile michezo yake na wazazi wake kabla ya chajio, yale matembezi ya kila Jumapili yote yakatoweka. Baba na mama wakawa wanarudi nyumbani baada ya saa nne usiku wakiwa wametoka kwenye masomo ya kuupigia msasa ujuzi wao; Jumamosi na Jumapili wana majadiliano na wanafunzi wenzao. Nyakati nyingine wazazi wote wawili walikuwa kwenye safari za kikazi. Nyakati kama hizi Tenga angepelekwa kwa shangazi ambako angekaa na kijakazi wake kwa wiki tatu; anaenda shuleni na kurudi huko huko kwa shangazi. Wahenga walisema kwamba, akosaye la mama hata la mbw a huamwa. Pengo la malezi lilfloachwa na wazazi wa Tenga lilijazwa na walezi wengine, wakiwemo vijakazi, shangazi, marika, walimu, majirani na hata vibonzo! Tenga alijifunza mengi kutokana na walezi hawa. Alifunzwa namna ya kupigana miereka, kutumia ujanja kujitoa katika matatizo, kutumia maneno makali kujihami alipochokozwa na wenzake, pamoja na mitindo mbalimbali ya kujinadhifisha. Mafunzo ambayo Tenga aliyapata, hasa kutoka kwa marika, yaliutia ila mwenendo na uhusiano wake na walimu. Darasani akawa haishi kuvuruga masomo kwani kila mara angetenda kituko iii mwalimu na wanafunzi waubaini uwepo wake. Vituko hivi vilisababisha kudorora kwa alama zake. Walimu wakajaribu kuurekebisha utundu wake lakini zikawa kama juhudi za mfa-maji. Tabia ya Tenga haikuwa ufa tena bali ukuta ambao ulihitaji kujengwa upya. Mkuu wa Idara ya Ushauri na Uelekezaji shuleni ilibidi ahusishwe. Akamhoji Tenga na kupambaukiwa kuwa vitendo vya Tenga vilikuwa na asili ambayo ilihitaji kuchunguzwa. Akampendekezea mwalimu wa darasa kuwashirikisha wazazi katika kutafuta mbinu za kumwelekeza Tenga zaidi. Bwana Mtanga na mkewe Zuhura walipoambiwa kuhusu hall ya Tenga walipigwa na bumbuazi. Hawakuwa wameyawazia madhara ya kutoshiriki kikamilifu katika malezi ya mtoto wao. Mwalimu aliwaambia ya kwamba nusura Tenga aingizwe na wenzake katika matumizi ya dawa za kulevya lakini akakataa na kusema kuwa hata babake hakujaribu kutumia kileo chochote. Wazazi waliona haya na kujilaumu. Hata hivyo walishukuru ya kwamba walimu waliyagundua matatizo haya kabla hayajaiangamiza familia yao. MASWAHILI: 41. Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa kifungu.Bwana Mtanga na Bi. Zuhura: A. walimlea Tenga kwa kushauriana, walikuwa mashuhuri; B. walimlea Tenga kwa kuchangamkiana, walikuwa maarufu; C. waliingiliana vyema na majirani, walipenda kusaidia; D. waliingiliana vyema na walimu,walipenda kutoa. 42. Utajiri wa wazazi. wa Tenga ulitokana na: A. uwajibikaji wao katika shughuli zao B. kupata vyeo katika madaraja tofauti tofauti; C. kupata shahada na stashahada mbalimbali; D. uwajibikaji wao katika taaluma zao. 43. Wazo kuu linalojitokeza katika aya ya line ni Kwamba: A. Jambo lolote likifanywa bila ushirikiano huweza kuleta madhara. B. Jambo Iolote likifanywa bila kipimo huweza kuleta madhara. C. Jambo lolote likifanywa bila utulivu huweza kuleta madhara. D. Jambo lolote likifanywa bila mtazamo huweza kuleta madhara. 44. Kifungu kinaonyesha kuwa ukosefu wa malezi bora husababisha: A. kupigana miereka daima iii kupata maslahi; B. kudhoofika kwa maadili; C. kuharibu masomo darasani ill kuonekana kote; D. kuharibika kwa urafiki. 45. “Tabia ya Tenga haikuwa ufa tena bali ukuta ambao ulihitaji kujengwa upya.”Ina maana: A. Tabia ya Tenga ilikuwa imeharibika kabisa kiasi cha kuhitaji kurekebishwa kikamilifu. B. Tabia ya Tenga ilikuwa imeharibika kabisa kiasi cha kuhitaji kushauriwa kikamilifu. C. Tabia ya Tenga ilihitaji kushughulikiwa kikamilifu. D. kuharibika kwa urafiki. 46. Kwa mujibu wa kifungu, Idara ya Ushauri na Uelekezaji inasaidia katika malezi kwa: A. kuwahoji vijana na kuwaita wazazi wao; B. kutambua matatizo ya vijana na kuonyesha mbinu za kuwashirikisha; C. kutambua matatizo ya vijana na kuangazia mbinu za kuyasuluhisha; D. kuwahoji vijana na kuwaambia matatizo yao. 47. Kulingana na aya ya mwisho, wazazi wa Tenga: A. Hawakujua umuhimu wa kuishi karibu na mtoto wao. B. Walipuuza umuhimu wa ushirka wa karibu na walezi wao. C. Walipuuza umuhimu wa ushirika wa karibu na mtoto wao. D. Hawakujua umuhimu wa kuishi karibu na walezi wao. 48. Chagua jibu linaloonyesha sifa za Tenga. A. mcheshi, mwenye kupenda wazazi; B. mwenye mapenzi ya dhati, anayetafuta kushirikishwa; C. mchangamfii, mwenye kupenda unadhifu; D. mwenye rnsimamo imara, anayetafuta kutambuliwa. 49′ Kisawe cha, `hakwenda nguu,’ ni: A. hakujitia kapuni; B. hakujitia hamnazo; C. hakufa moyo; D. hakufa Kikondoo. 50. Maana ya, `kujihami’, kwa mujibu wa kifungu ni: A. kujitetea; B. kujinasua; C. kujihadhari; D. kujizatiti. Loading … Question 1 of 50