STD 8 KISWAHILI TEST2

Please enter your email:

Kiswahili ni mojawapo ya lugha………….1…………wazungumzaji wengi. Lugha ya Kiswahili     …………..2……. zama za ukoloni…………3……..Waafrika dhidi ya wakoloni. Hatua ya kukifanya Kiswahili lugha rasmi nchini Kenya ……..4………..hadhi ya lugha husika.    ………..5……………hapo awali, tunatarajia Kiswahili kutumiwa  ………6………… na Kiingereza katika shughuli za kiofisi. Hata hivyo,  ……………7…………  patakuwa na haja ya kutafsiriwa kwa makala mengi kwa Kiswahili.

1.MAJIBU

 
 
 
 

2. MAJIBU

 
 
 
 

3. MAJIBU

 
 
 
 

4. MAJIBU

 
 
 
 

5. MAJIBU

 
 
 
 

6. MAJIBU

 
 
 
 

7. MAJIBU

 
 
 
 

Mtoto ana haki  ………8…….. Anastahili …..9……… vizuri iii kuifaa jamii  ……..10….. Tabia ya mtoto  ……….11……. na jamii, hivyo tunaweza kudai kuwa mtoto ni zao la jamii. ……12……. mtoto ana haki ya lishe bora  ……13……nguvu, yaani,……14….., na kumwezesha kujikinga na maradhi kama vile ……..15…... Ugonjwa huu husababishwa na kula chakula ambacho kina upungufu wa viinilishe.

8.MAJIBU

 
 
 
 

9. MAJIBU

 
 
 
 

10. MAJIBU

 
 
 
 

11. MAJIBU

 
 
 
 

12. MAJIBU

 
 
 
 

13. MAJIBU

 
 
 
 

14. MAJIBU

 
 
 
 

15. MAJIBU

 
 
 
 

Kutoka swali la 16 rnpaka 30, chagua jibu lililo sahihi.

16. Maneno yafuatayo yanafuatana vipi katika kamusi?

(i) muhibu   (ii) muhtasari     (iii) muhali      (iv) muhula

 
 
 
 

17. Umoja wa: “Nywele zao ndefu ziliwavutia.” ni:

 
 
 
 

18. Chagua jibu lenye nomino zilizo katika ngeli ya i-i pekee.

 
 
 
 

19. Ni jibu lipi lenye maelezo sahihi?

 
 
 
 

20. Hisani ni kwa wema na kunadi ni kwa:

 
 
 
 

21. Chagua kinyume cha: Wageni waliwasili kabla ya eropleni kupaa.

 
 
 
 

22. Tikiti, limau na fenesi ni matunda ilhali wimbi, mahindi na mtama ni:

 
 
 
 

23.  6/9 kwa maneno

 
 
 
 

24. Kukanusha kwa: “Nyungu iliyonunuliwa iliuzwa   tena,” ni:

 
 
 
 

25. Ni jibu lipi ambalo si aina ya shairi?

 
 
 
 

26. Onyesha sentensi yenye kielezi cha

 
 
 
 

27. Kiambishi `ka’ katika sentensi: “Alienda shuleni  akasome Kiswahili;” kinaonyesha:

 
 
 
 

28.  Chagua kundi Iinaloonyesha kitenzi .kilichoundwa kutokana na kivumishi.

 
 
 
 

29.  Kitara ni upanga mwembamha wa kuongozea gwaride. Kitara vile vile ni:

 
 
 
 

30. Chagua sentensi ambayo imetumia `na” kama  kiunganishi.

 
 
 
 

Soma kifingu kifilatacho kisha ujihu maswali 31 mpaka 40

Kuna aina mbili kuu za misitu. Ipo ile ya kiasili kama vile Msitu wa Karura na Msitu wa Mau. Hali kadhalika, ipo misitu ya kupandwa kama ile ya Kinale na Webuye. Misitu ni hazina kubwa kwa jamii yoyote ile. Kila mwanajamii anapaswa kujivunia misitu.

Misitu husheheni miti ya aina nyingi ambayo, pamoja na kuwa makazi ya wanyama, hutoa vyakula kama vile matunda na majani ambayo huwafaidi binadamu na viumbe wengine. Bila misitu binadamu na wanyama wangeangamia.

Misitu ni kivutio cha watalii. Watalii kutoka ndani na nje ya nchi huzuru misitu na mbuga mbalimbali za wanyama kuajabia uzuri wake. Watalii hawa hulipa fedha za kigeni ambazo hutumiwa kuanzishia miradi ya kiuchumi kama vile kustawisha miundomsingi.

Fauka ya hayo, misitu husafisha hewa na kurembesha mandhari wanamoishi binadamu. Rangi ya kijani kibichi na maua yenye rangi tofautitofauti huyafanya mazingira kupendeza hata yakitazamwa kwa mbali. Mandhari yasiyo na miti hayakosi urembo tu, bali huwa wazi kiasi kwamba hata mapaa ya majengo yaliyo hapo wakati mwineine hupeperushwa na upepo mkali.

Vipindi virefu vya jua huwanyima viumbe starehe na huweza kusababisha saratani ya ngozi kwa binadamu. Miti hufanya vivuli ambavyo huwakinga watu na wanyama dhidi ya miale ya jua. Isitoshe, si ajabu kuwa mahali ambapo pana miti mingi kwa kawaida hupata mvua hata wakati usio wa majira ya mvua kwingineko.

Sekta ya tiba imefaidika si haba kutokana na miti. Matabibu wa kienyeji na hata wa kisasa hutumia mizizi, majani na magome ya miti kutengenezea dawa. Miti kama vile mwarubaini hutibu magonjwa mengi. Hivi rasa magonjwa kama vile bolisukari, shinikizo la damu na ugonjwa wa figo yarneweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa zinazotokana na miti. Inasemekana kuwa hata nyoka humtibu nyoka mwenzake kwa majani!

Miti hutumiwa viwandani kutengenezea bidhaa kama vile karatasi na samani. Viwanda hivi hutoa ajira kwa maelfu ya raia, hivyo kupunguza makali ya uhaba wa nafasi za kazi nchini.
              Ni wazi kuwa uhifadhi wa misitu una manufaa tumbi nzima kwa binadamu. Hata hivyo, binadamu mwenyewe ndiye anayeiangamiza misitu yenyewe. Watu wenye mate ya fisi wamekata miti kiholela kwa ajili ya kupata kuni na kuchomea makaa ya kuuza. La kusikitisha ni kwamba watu hawa hawadiriki kupanda miti mingine kufidia ile waliyoikata. Wengine, kwa kutojua wanajipalia makaa, hupanda miti ambayo inakausha vyanzo vya maji na kuchangia kuenea kwa kasi kwa jangwa. Hali kadhalika, wapo warina asali ambao katika juhudi zao za kurina husababisha kuteketea kwa misitu.

Kifungu cha katiba kinachohusu mazingira na mali ya asili kinasisitiza suala la uhifadhi wa mazingira. Kila mwanajamii basi ana jukumu la kuilinda misitu na kuepuka mazoea ambayo yanaiangamiza, la sivyo tutakuwa tunajichimbia kaburi.

MASWALI

31. Kulingana na kifungu, mchango wa utalii  kwa jumla ni:

 

 
 
 
 

32. Chagua hasara za kutohifadhi misitu kwa mujibu wa kifungu.

 
 
 
 

33. Ni jibu lipi sahihi kulingana na kifungu?

 
 
 
 

34. Kifungu kinasema kuwa miti hutumiwa:

 
 
 
 

35. Manna ya methali, “Mwiba wa kujichoma  hauambiwi pole,” imedhihirika katika kifungu kwa vile:

 
 
 
 

36. Mwandishi anaonyesha kuwa kichocbeo  kikuu cha kukata miti ni:

 
 
 
 

37. Ni jibu lipi ambalo si sahihi kulingana na  aya ya nane?

 
 
 
 

38. Kulingana na aya ya mwisho:

 
 
 
 

39. Kwa mujibu wa taarifa, `yameweza  kudhibitiwa’, ina manna:

 
 
 
 

40. Manna ya, `hawadirikr, kulingana na kifungu ni:

 
 
 
 

Soma kifingu kifuatacho kisha ujthu maswali 41 mpaka 50. 

Tenga alilelewa katika mazingira yaliyojaa neema, furaha na uchangamfu. Wazazi wake Bwana Mtanga na Bi. Zuhura walikuwa wakwasi wa kutajika katika janibu hizo, si kwa mali tu bali kwa nyoyo zao zilizokuwa tayari kila mara kuwakirimu wanalujiji kwa lolote.

Bwana Mtanga na Bi. Zuhura hawakulala maskini wakaamka matajiri. Mtanga alianza kazi kama tarishi katika Makavazi ya Umma. Ingawa hii ilikuwa kazi ya kijungu jiko mekoni, Mtanga hakwenda nguu; alijitahidi kwa vyovyote vile kujinyanyua. Akajisajili kwa kozi mbalimbali za usimamizi wa makavazi na kuhitimu vyeti tofautitofauti vikiwemo stashahada na shahada katika masuala ya usimamizi wa mashirika ya umma. Jitihada zake zikazaa matunda. Akapandishwa cheo mwaka baada ya mwingine hadi akawa msimamizi wa Makavazi ya Umma. Baadaye akaajiriwa na shirika la Msalaba Mwekundu kama Mkrurugenzi wa Huduma za Kijamii.

Bi. Zuhura naye, baada ya kuhitimu masomo ya shule ya upili, alisomea taaluma ya ukutubi na baadaye kuajiriwa katika maktaba ya chuo kikuu cha Tungama. Hapa Zuhura alitambua kuwa amepata nafasi adimu ya kuutia makali ubongo wake. Akajisajili kwa kozi ya ukutubi na kuhitimu shahada ya daraja la kwanza katika taaluma hii. Wakuu wake kazini wakavutiwa na juhudi zake na kumpandisha cheo, akawa Mkutubi Mkuu.

Wakati Bwana Mtanga na Bi. Zuhura walipokuwa wakijiendeleza kitaaluma na kiuchumi, Tenga naye alikuwa anajikulia tu kama uyoga bila mpalilizi. Nyadhifa za wazazi wake zilimpokonya Tenga ushirika wa wazazi wake. Ile michezo yake na wazazi wake kabla ya chajio, yale matembezi ya kila Jumapili   yote yakatoweka. Baba na mama wakawa wanarudi nyumbani baada ya saa nne usiku wakiwa wametoka kwenye masomo ya kuupigia msasa ujuzi wao; Jumamosi na Jumapili wana majadiliano na wanafunzi wenzao. Nyakati nyingine wazazi wote wawili walikuwa kwenye safari za kikazi. Nyakati kama hizi Tenga angepelekwa kwa shangazi ambako angekaa na kijakazi wake kwa wiki tatu; anaenda shuleni na kurudi huko huko kwa shangazi.

Wahenga walisema kwamba, akosaye la mama hata la mbw a huamwa. Pengo la malezi lilfloachwa na wazazi wa Tenga lilijazwa na walezi wengine, wakiwemo vijakazi, shangazi, marika, walimu, majirani na hata vibonzo! Tenga alijifunza mengi kutokana na walezi hawa. Alifunzwa namna ya kupigana miereka, kutumia ujanja kujitoa katika matatizo, kutumia maneno makali kujihami alipochokozwa na wenzake, pamoja na mitindo mbalimbali ya kujinadhifisha.

Mafunzo ambayo Tenga aliyapata, hasa kutoka kwa marika, yaliutia ila mwenendo na uhusiano wake na walimu. Darasani akawa haishi kuvuruga masomo kwani kila mara angetenda kituko iii mwalimu na wanafunzi waubaini uwepo wake. Vituko hivi vilisababisha kudorora kwa alama zake. Walimu wakajaribu kuurekebisha utundu wake lakini zikawa kama juhudi za mfa-maji. Tabia ya Tenga haikuwa ufa tena bali ukuta ambao ulihitaji kujengwa upya. Mkuu wa Idara ya Ushauri na Uelekezaji shuleni ilibidi ahusishwe. Akamhoji Tenga na kupambaukiwa kuwa vitendo vya Tenga vilikuwa na asili ambayo ilihitaji kuchunguzwa. Akampendekezea mwalimu wa darasa kuwashirikisha wazazi katika kutafuta mbinu za kumwelekeza Tenga zaidi.

Bwana Mtanga na mkewe Zuhura walipoambiwa kuhusu hall ya Tenga walipigwa na bumbuazi. Hawakuwa wameyawazia madhara ya kutoshiriki kikamilifu katika malezi ya mtoto wao. Mwalimu aliwaambia ya kwamba nusura Tenga aingizwe na wenzake katika matumizi ya dawa za kulevya lakini akakataa na kusema kuwa hata babake hakujaribu kutumia kileo chochote. Wazazi waliona haya na kujilaumu. Hata hivyo walishukuru ya kwamba walimu waliyagundua matatizo haya kabla hayajaiangamiza familia yao.

MASWAHILI:

 

41. Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa kifungu.Bwana Mtanga na Bi. Zuhura:

 
 
 
 

42. Utajiri wa wazazi. wa Tenga ulitokana na:

 
 
 
 

43. Wazo kuu linalojitokeza katika aya ya line ni  Kwamba:

 
 
 
 

44. Kifungu kinaonyesha kuwa ukosefu wa  malezi bora husababisha:

 
 
 
 

45. “Tabia ya Tenga haikuwa ufa tena bali ukuta ambao ulihitaji kujengwa upya.”Ina maana:

 
 
 
 

46. Kwa mujibu wa kifungu, Idara ya Ushauri na Uelekezaji inasaidia katika malezi kwa:

 
 
 
 

47. Kulingana na aya ya mwisho, wazazi wa Tenga:

 
 
 
 

48. Chagua jibu linaloonyesha sifa za Tenga.

 
 
 
 

49′ Kisawe cha, `hakwenda nguu,’ ni: 

 
 
 
 

50. Maana ya, `kujihami’, kwa mujibu wa kifungu ni:

 
 
 
 

Question 1 of 50